Maisha yangu hapa Norvege
Sikiliza uzoefu(experience) ya Honoratte na usome kuhusu jamii(societe) ya Norway kwa Kiswahili
Nilifika Norway nikiwa mtu mzima (umri wa miaka 33) nikiwa na watoto 2 na mume wangu wa wakati huo. Nilipata wengine watoto 5 hapa Norway, nilipitia misiba mikubwa, lakini sikukata tamaa.
Ni nini unahitaji kufanya sasa?
Tafuta shirika(organisation) katika eneo unaishi emo na ujiandikishe kutumika bila malipo. Itakusaidia kujifunza lugha, kupata mtandao(reseaux sociaux), na ni fungulo ya kupata kazi. Unaweza kutizama kwenye frivillig.no hata kama haujui lugha. Unaweza kutembelea site web ya mashirika ya hiari (volontaire) au kuuliza muhusika(responsable wako) kwenye centre ya mapokezi ya wakimbizi.
Kutafuta kazi ni mtihani mkubwa
Kabla ya kupata kazi, nilikuwa nimetuma maombi (demandes d’emplois) kama 100. Usivunjike moyo. Ukipata tu kazi yako ya kwanza apa, unapata pia uzoefu( experience) ambayo itakusaidia kupata kazi bila usumbufu unapotuma maombi(demande) ya kazi wakati ujao. Na pia unapata mtandao mkubwa wa watu ambao wanaweza kukuambia kuhusu kazi nyingine wakati ujao. Soma zaidi kwenye tovuti(site web) hii.
Kupata mtu wa reference apa Norvege
Wapana ma kazi hawaangaliye sana uzoefu(experience) wa kazi ambao unawo tokea inchi mwako,wanaangalia sana uzoefu wako wa kazi apa Norway.
Usisahau kabisa kujifanyia ma references za muzuri ku kazi yako apa, na izo references uzichunge muzuri kwaju ya matumizi ya baadaye. Ni bora ukiwa na mtu reference mwenye anajuwa muzuri Norvege na utamaduni(culture) wake.
Mabadiliko yanaweza kufanyika sasa
Mda muzuri wa kuanza mabadiliko ni sasa. Waza kwanza nini unataka ufanye, ndoto gani uko nazo. Uanze kujituma sana kwa ajili ya ndoto zako. Je unaweza kujifunza lugha sasa? Ndio unaweza. Ukitumia sana neno eti haiwezekani, unakuwa umesimamisha maendeleo yako mwenyewe kwa ngambo ya masomo na ki kazi.
Honoratte anatokea Kongo
Sikia jinsi nilivyoweza kushinda changamoto kwa kujitolea, kujifunza lugha na ku assumer ma chaguo zangu. Ilikuwa ni hatua ya mabadiliko kwangu mu kupanua mtandao wangu (reseau social), kutafuta na kudumu mu kazi, kunijengea ujasiri na kujifunza kuweka mipaka. Nilipata kujifunza kanuni za kijamii (codes sociaux) na daima kupata ujasiri wa kufanya juhudi, hata wakati jamii haikuwa katika uwezo wangu.
Trykk på CC i verktøylinja på filmen for å endre undertekst
Mikutano ya uzoefu (expérience) kwenye mitandao.
Tazama matangazo kwenye Youtube au Facebook kwa mazungumzo kutoka kwa watu walio na experiences za muzuri kuhusu kuji integrer. Hapo chini unaona matangazo yetu matatu kwa Kiswahili ambapo Honoratte ni mtangazaji.
Publisert Torsdag 11.11.21 kl. 14.00
Uzoefu (experiences) ya kuwa mpya nchini Norway
Publisert Torsdag 18.11.21 kl. 14.00
Mtandao wa kijamii na mafunzo ya Kinorwe
Publisert Torsdag 25.11.21 kl. 14.00
Njia(processus) ya mtu kupata kazi
Biblioteque
Habari za maana kuhusu kazi, masomo na jamii(societe) ya Norvege kwa kiswahili.(Iko inatengenezwa)